KOMBORA LA HATARI ZAIDI ULIMWENGUNI KWA SASA

Imeandikwa na Josephat Keraryo Nyambeya kwa msaada wa mitandao wa kijeshi ya China na Marekani. 

Kombora la DongFeng-41 (DF-41) ni kombora linalotengenezwa na kutumiwa na jeshi la China. Ni kombora la masafa marefu (mabara)., kwa kimombo waweza liita Inter Continental Ballistic Missile (ICBM).
DF-41 ICBM with Range of 14,000 km, Able to Break Through US Anti-missile Network and hit all targets in Europe and the US


Lina uwezo wa kusafiri umbali wa kati ya Km 12,000 hadi 15,000. Umbali huu unaoweza fikiwa na DF-41 unalifanya kuwa kombora linaloenda masafa marefu kuliko yote duniani na kulizidi lile la Marekani Minutemen LGM-30, ambalo lina uwezo wa kufika Km 13,000. Km 13,000 ni sawa na umbali wa Dar Es Salaam hadi New York ni Km 12,400 hivyo nadhani unaweza ona uwezo wa makombora haya.  Yaani kwa maana nyingine makombora haya ya wababe hawa yanaweza fyatuliwa kutoka ncha ya kaskazini mwa dunia yakafika ncha ya kusini mwa dunia bila shaka yoyote maana umbali kati ya hizo ncha mbili ni Km 12,430. Makombora ya ICBM yana uwezo wa kugonga pembe yoyote ya dunia bila shaka yoyote. Unaweza kulifyatua ukiwa chumbani kwako likaenda kutua Sydney kule Australia bila wasi wasi. (anyway tuendelee).


Kombora la DF-41 ndilo kombora linaloaminika kuwa na kasi kubwa kuliko makombora yote duniani, likiaminika kusafiri kwa kasi ya Km 30,626 kwa saa sawa na Maili 19,030 kwa saa au sawa na Km 8.5073 kwa sekunde. Hii ikiwa na maana ya kwamba kombora hili linaweza kutoka Mbezi Africana  jijini Dar Es salaam hadi ikulu ya Dar kwa sekunde moja. Historia ya kuundwa kwa kombora hili ilikuwa mahsusi ili kupambana na nguvu ya kijeshi na nyuklia ya Marekani.
Image result for DF-41

Kombora la DF-41 lilijaribiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012.


SIFA ADIMU ZA DF-41

1.       Lina uzito wa tani 80
2.       Lina urefu wa mita 21 na upana wa mita 2.25
3.        



Toa maoni yako juu ya habari hii. Pia usisahau kubonyeza matangazo yaliyopo juu na chini hata pembeni ya habari hii maana ndio wadhamini wanaonipa nguvu ya kuendelea kuandika, bila wao sitaweza kuandika. 



OPARESHENI YA KUWAOKOA MATEKA UGANDA ILIYOFANYWA NA JESHI LA ISRAEL

entebbeairport.jpg
Imeandikwa na Josephat Keraryo Nyambeya kwa msaada mkubwa wa mitandao.




Oparesheni Entebbe ni operesheni ya kuokoa mateka wa Kisrael waliotekwa na magaidi , oparesheni hii ilifanywa na makomando wa Israel (IDF) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe tarehe 4 July 1976, wiki moja kabla yaani tarehe 27 June ndege ya shirika la Air France ikiwa na abiria 248 ilitekwa na wanachama wawili wa chama cha vuguvugu a ukombozi wa Palestina (PFLP-EO) baada ya amri ya mtu aliyefahamika kama Wadie Haddad, pia katika utekaji huo kulikuwa na wanachama wawili wa vuguvugu za kimapinduzi huko Ujerumani.


Watekaji walikuwa wanadai Israel iwaachie huru wafungwa 40 na wengine 13 waliokuwa wamefungwa kwenye magereza mbalimbali nchini humo ili iwaachie mateka hao. Ndege hiyo iliyoanzia safari yake mjini Tel-Aviv nchini Israel ikiwa inatarajiwa kutua jijini Paris-Ufaransa ilibadilishwa uelekeo na kushuka jijini Athens-Ugiriki kwa ajili ya kujaza mafuta kabla haijapaa kuelekea Benghazi-Libya kasha Entebbe uwanja mkuu wa ndege nchini Uganda.


Serikali ya Uganda ilikuwa inawasapoti watekaji hao, na binafsi dikteta Idd Amin aliwakaribisha watekaji hao (huyu Idd Amin akili zake zilimtosha mwenyewe). Baada ya kuwaondoa mateka wote kutoka uwanjani na kuwapeleka kwenye jengo lililokuwa halitumiki hapo uwanjani, watekaji waliwatenganisha Waisrael na wasio Waisrael .
Siku mbili baadae mateka 148 ambao hawakuwa raia wa Israel waliachiwa na kurejea jijini Paris. Raia 94 wa Israel ikiwemo na wafanyakazi 12 wa shirika hilo la ndege waliachwa kama mateka na kutishiwa kuawawa .

mossad 1.jpg
Jeshi la Israel (IDF) lilizipata taarifa walizopewa na shirika la Ujasusi la nchi hiyo Mossad juu ya tishio la mateka hao kuuliwa kama Israel haitatii matakwa ya watekaji hao ambayo yalikuwa kuwaachia huru wafungwa wote wa Kipalestina waliokuwa kwenye magereza nchini humo. Kitisho hiki kilipelekea IDF kupanga misheni ya Uokozi, operesheni hii ilipangwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na Mapambano kutoka Jeshi la Uganda maana walijua fika kuwa endapo watafanikiwa kuingia Uwanja wa Entebbe kwa ajili ya uokoaji huo lazima wangekabiliana na upinzani kutoka jeshi la Idd Amini hivyo walijiandaa kwa ajili ya hilo.


Oparesheni ilifanyika usiku , Israel ilichukua ndege iliyobeba makomandoo 100 na kusafiri zaid ya Maili 2500 (Kilomita 4000) kuelekea Uganda kwa ajili ya uokozi. Oparesheni iliyochukua wiki nzima kuiandaa ilipangwa kuchukua dakika tisini tu kukamilika, Mateka 102 waliokolewa , makomando watano wa Israel walijeruhiwa, Kamanda aliyekuwa akiongoza Operesheni hiyo Lt. Kanali Yonathan Netanyahu aliuwawa. Watekaji wote, mateka watatu, na wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda waliuliwa . Pia ndege vita 11 za jeshi la Uganda ziliharibiwa.


Opareheni hii iliyopewa jina la fumbo (codename) la Oparesheni Thunderbolt, mara nyingine huitwa oparesheni Yonathan kama kumbukumbu ya Kiongozi aliyeiongoza oparesheni hii. Kiongozi wa oparesheni hii alikuwa kaka mkubwa Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa sasa wa Israel.
Katika uwanja wa ndege wa Entebbe watekaji wane waliungana na wenzao wanne wakiwa wanapewa sapoti na Jeshi la Uganda. Idd Amini alikuwa akiwatembelea mateka kila siku na kuwapa maendeleo ya mazungumzo juu ya kile kilichokuwa kikiendelea, na kuwaahidi kuachiwa huru kama maafikiano yatafikiwa. Tarehe 28 siku moja baada ya utekaji watekaji walidai fidia ya dollar Millioni 5 ili waiachie ndege na pia wapalestian 53 waliokuwa wamefungwa kwenye magereza ya Israel wachiiwe huru. Walidai kama madai yao hayatatekelezwa wataanza kuwaua mateka kuanzia tareh 1 July mwaka huo wa 1976.


Wiki hiyo Israel ilijaribu kutumia majukwaa ya kisiasa ili kuwaokoa mateka. Vyanzo vingi vinadai baraza la Mawaziri la Israel lilipanga na kukubaliana kuwaachia wafungwa hao wa Kipalestina ili kuokoa roho za waisrael hao waliotekwa. Burka bar-Lev afisa mstaafu wa jeshi la Israel alikuwa anamjua Idd Amin kwa mda mrefu alipewa jukumu la kumbembeleza Idd Amin ili awaachie mateka hao, Bar-lev alikuwa akimpigia simu mara nyingi Idd Amin kumuomba awaachie mateka bila mafanikio, Idd Amin hakuelewa somo. Israel iliomba Marekani kuongea na rais wa Misri Anwar Sadat aliyekuwa na mahusiano mazuri na Idd Amin kumuomba awaachie mateka bila mafanikio. Sadat alijaribu kuongea na PLO na seriakli ya Uganda , pia Mwenyekiti wa PLO wa kipindi hicho Yasser Arafat alituma ujumbe wake nchini Uganda kuongea na watekaji ila watekaji walikataa katakata kuonana na mjumbe huyo aliyetumwa.
Tarehe ya mwisho ilifika (yaani tarehe 1, July) na hapo baraza la mawaziri la Israel liliomba watekaji kusogeza mda hadi tareh 4 ili waweze kukubalina . Idd Amin pia aliwaomba wasogeze siku hadi tarehe hiyo hadi arudi kutoka kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika (Kipindi hicho OAU) alipokuwa anaenda kukabidi Uenyekiti wa mkuu mwingine wan nchi.


Kukubaliwa kwa ombi hili kuliwafanya Waisrael kujipanga zaidi jinsi ya kuifikia Entebbe. Tarehe 3 July saa 12:30 jioni Baraza la mawaziri la Israel lilibariki kufanyika kwa oparesheni hii, utekelezaji wa Oparesheni hii ukiwasilishwa na Meja Jenerali Yekutiel Kuti Adam na Brigedia Jenerali Dan Shomron mbele ya baraza hilo.


Mwanzoni operesheni ilipangwa kwa kuwadondosha makomando wa Kiyahudi ndani ya ziwa Vicktoria na kuwaacha watumie boti za mipira hadi kwenye ncha ya uwanja wa ndege wa Entebee ulipo pembezoni kabisa mwa Ziwa Vicktoria. Walipanga kuwauwa watekaji wote na kuwaokoa mateka, ila baadae Israel iliukaaa mpango huu kwa sababu ya kuwa walipata taarifa kuwa Ziwa Vicktoria lina mamba wengi hivyo ingekuwa hatari kwa mateka waliokolewa.


Wakati wakipanga oparesheni hiyo walijiuliza watajazia mafuta wapi kwenye ndege yao waliyopanga kuitumia kufika Entebbe, walikosa ndege ya kuweza kufika Entebbe na kurudi Israel bila kujazwa mafuta, hivyo kitu hicho kikawaumiza kichwa tena. Walipanga kuongea na moja ya mataifa ya Afrika ya Mashariki ili kuweza kuwaruhusu kutumia uwanja wao wa ndege kwa ajili ya ndege yao kutua na Kujaza mafuta. Katika kuitafuta nchi ambayo ingewakubalia ombi lao wakaamua kuichagua Kenya na kuwatuma mabalozi wake waliokuwepo nchini Kenya pamoja na wafanyabiashara wa Kiyahudi wenye ushawishi mkubwa nchini Kenya kwenda kuongea na Rais Jomo Kenyatta juu ya ombi lao hilo, msomaji naomba ufahamu kuwa Tanzania haikuwa na uhusiano mzuri na Israel kwa hiyo njia pekee iiyokuwepo ni kuitumia Kenya.


Oparesheni hii isingeweza kufanikiwa bila msaada wan chi yoyote ya Afrika Mashariki, waliotumwa kwa Kenyatta walibubujikwa na machozi ya furaha baada ya ombi lao la kuutumiwa uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kukubaliwa. Kenyatta pia aliwaruhusu MOSSAD kuitumia Kenya kama njia ya kukusanya taarifa za kiintalenjesia.


Mossad ilipata picha kamili ya mahali walipo mateka, idadi ya watekaji pia walizipata taarifa za juu ya uhusikaji wa Jeshi la taifa la Uganda kutoka kwa wale mateka walioachiwa na kurudi Paris (moja ya udhaifu wa watekaji hawa). Taarifa za mateka hao waliochiwa zililisaidia sana Jeshi la Israel na Mossad kujua idadi ya kikosi watakachokituma Entebbe.


Kama bahati ya mtende kuota Jangwani Mossad pia ilipata taarifa za kuwa kuwa Uwanja huo wa ndege wa Enttebe ulijengwa na kampuni moja la Kisrael mnamo mika ya sitini, hivyo iliwasiliana na kampuni hilo liitwalo Solel Boneh na kupata ramani kamli ya uwanja huo na majengo yaliyopo uwanjani hapo.
Kikosi kazi kikiwa na Makomandoo wapatao 100 na silaha nzito nzito walijindaa kuelekea Uganda. Kikosi kazi hizi kiligawanyika katika vitengo vitatu.


Moja, kamandi ya Ardhini iliyoongozwa na Brigedia dan Shomron na muwakilishi wa Kikosi cha anga Kanali Ami Ayalon, kikosi hiki kilikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha ulinzi unaimarishwa uwanjani hapo pamoja na kuyakata mawasiliano yote kutoka uwanjani hapo. Kikosi cha pli kikiongozwa na Kamanda kijana wa miaka 29 tu Luteni Kanali Yonathan Netanyahu kikosi hiki kilikuwa na makomando kutoka kambi ya Sayeret Matkal kilipewa kazi ya kuuteka uwanja wa ndege wa kuingia kwenye terminal na kuwaokoa mateka, Meja Betser alichukua nafasi ya kukiongoza kikosi hiki baada ya Yonathan kuuwawa kwa risasi. Kikosi kazi kingine kilipewa jukumu la kuzilinda njia za Kutulia ndege (runways-siko vizuri Kiswahili mnisamehe) na kulinda sehemu ya kujazia mafuta na kuhakikisha ndege za Israel zinajaza mafuta uwanjani hapo kabla ya kupaa (Yaani hii ni sawa na kuvamiwa na Majambazi ukiwa umelala na mkeo wewe unainamishwa nay eye anainamishwa mbele yako). Kikosi hiki kiliongozwa namakamanda watatu walikouwa na majukumu tofauti, kikosi hiki pia kilipewa jukumu la kuharibu ndege vita zote za jeshi la Uganda zilizokuwepo uwanjani hapo.


Kikosi hiki makini cha makomando wa kiyahudi kilipaa kutoka Sharm el-Sheikh ndege iliyowabeba makamanda hawa ikiwa inaruka umbali wa Mita 30 (futi 100) tu ili kuepuka kunaswa na Rada za Sudan, Misri na Saudi Arabia (kwa wataalamu wa RADAR nadhani watakubaliana na mimi) kilipita bahari ya shamu kuelekea Kusini na kasha kupita Djibouti kutoka huko walitua uwanja wa ndege jijini Nairobi, wakiwa na ndege mbili za Boeing 707 ndege moja ikiwa ikiwa imebeba madawa na vifaa tiba na ndege ya pili kikiwa imewabeba makamanda.


Jeshi la Israel lilitua uwanja wa Entebbe saa tano kamili usiku July 3, ndege ya mizigo ikiwa tayari imefunguliwa milango gari nyeusi aina ya Mercedes Benz iliyofanana na ile aliyokuwa anatembelea rais Idd Amin ilishuka kutoka kwenye ndege ikiwa imeambatana na Land Rovers kadhaa sawa na zile zilizokuwa zinampa Idd Amin eskoti, walizitumia hizi kupita check points zote za uwanjani hapo. Ndege ya pili iliyowabeba makamanda wa kazi ilitua dakika sita baadae na hapo hapo wakayadandia magari hayo kuelekea kwenye jengo walipo mateka wakiwa wanafanana sawa sawa kabisa na Idd Amin, wakiwa wamekaribia terminal ya pili Maaskari waliokuwa guard wakiwa wanatambua kabisa kuwa Idd Amin alikuwa siku chache zilizopita alikuwa kanunua Mercedes nyeupe na kuachana na ile nyeusi walisimamisha msafara huo, makomando hao waliwafiatulia risasi kwa kutumia bastola za sailensa lakini hawakuwaua lakini komando mmoja aliyekuwa kwenye rand Rover za msafara aliwamalizia kwa kutumia bunduki kubwa isiyotoa sauti.


Wakiwa wameingia kwenye jengo lililokuwa linawafuga mateka hawa makomando walipaza sauti kutumia Vipaza sauti wakisema kwa Kingereza na Kiebrania kuwa “KAA CHINI, KAA CHINI” sisi ni wanajeshi wa Israel , kijana wa Kiyahudi wa miaka 19 alijaribu kusimama na alipigwa risasi kwa kudhaniwa kuwa alikuwa mtekaji. Pia mzee wa miaka 52 aliuwawa kimakosa baada ya kujeruhiwa na risasi ya jeshi la nchi yake, pia mateka mmoja mwenye asili ya Urusi aliuuliwa kwa risasi ya watekaji.
Wakiwa wanaendelea na oparesheni hii makamanda wa kiyahudi waliwauliza mateka kwa kiebrania walipo watekaji wengine na waliwaonyesha kwa vidole kuwa watekaji hao wamejificha kwenye chumba kinachofuata, makomandoo walikibomoa chumba hicho kwa magruneti kabla ya kuingia ndani na kuwamiminia risasi watekaji hao wa Kipalestina.


Kipindi wakiendelea a zoezi hilo la uokozi ndege vita tatu aina ya C-130 zilitua uwanjani hapo ili kutoa ulinzi wa anga ikiwa pia na kuzilinda ndege za jeshi la israel zikiwa zinajaza mafuta uwanjani hapo, oparesheni ya kuwaokoa mateka pia ilienenda sambamba na kuziharibu ndege za jeshi la Uganda zilizokuwepo uwanjani hapo.


Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka kwenye ndege zao wanaeshi wa Uganda waliendelea kurusha risasi, wanajeshi hawa wa Uganda wakiwa wanarusha risasi kutoka mnara wa kuongozea ndege walifanikiwa kuwajeruhi makomando watano na kumuua Kiongozi mmoja wa oparesheni Luteni Kanali Yonathan Netanyahu, makomando wa Israel walirusha RPG (wanaojua dhana za kijeshi RPG siyo jina geni kwao) na kuuharibu kabisa mnara huo wa kuongozea ndege, kulingana na mmoja wa vijana wa Idd Amin askari aliyempiga risasi Yonathan Netanyahu aliuliwa katika majibizano hayo ya risasi.
Zoezi hili lilichukuwa dakika 53 pekee japo lilipangwa kuchukua dakika 90. Katika oparesheni hii jumla ya wanajeshi 45 wa Uganda waliuliwa, mateka wote wanane waliuliwa, komando mmoja wa Israel alikufa, pia makomando 5 kujeruhiwa, ndge vita 11 za jeshi la Uganda aina ya Mig-17s na Mig-21 zilliharibiwa, pia kati ya mateka 106 mateka 3 waliuwawa kama nilivyoelezea mwanzoni pia na mateka mmoja kikongwe wa miaka 75 alisahaulika Uganda kikongwe huyu alichukiliwa nakupelekwa hospitali ya taifa ya Uganda-Mulago ambapo aliuliwa na wanajeshi wa Uganda kesho yake akiwa kitandani .
Ni hayo tu kwa leo, sina mengi ya kueleza juu ya oparesheni hii ila hayo kiduchu ninaamini yamekufanya uipate picha juu ya kile kilichotokea miaka 40 iliyopita. Ninaweza nikawa sijaandika kwa mtiririko mzuri ila nadhani hoja yangu imefika na imeeleweka.



Toa maoni yako juu ya habari hii. Pia usisahau kubonyeza matangazo yaliyopo juu na chini hata pembeni ya habari hii maana ndio wadhamini wanaonipa nguvu ya kuendelea kuandika, bila wao sitaweza kuandika. 





MFAHAMU JENERALI NORRIEGA NA JINSI ALIVYOTUMIWA NA MAREKANI KUITAWALA NCHI YA PANAMA NA KUFANYA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

General Manuel Antonio Norriega



upload_2017-7-31_16-13-43.png
Manuel Antonio Noriega Moreno (Spanish pronunC.I.A.tion: [maˈnwel noˈɾjeɣa]; February 11, 1934 – May 29, 2017) alikua mwanasiasa na mwanajeshi wa nchi ya Panama pia infoma wa C.I.A. wa kipindi kirefu. Alikua mtawala wa kijeshi wa Nchio ya Panama na dikteta 1983 mpaka 1989 wamarekani walipovamia nchi hiyo kijeshi na kumuondoa madarakani.

Alizaliwa jijini Panama na kusoma katika moja ya shule za kijeshi mjini lima na baada ya hapo ya sekondari ya Americans. Baada ya hapo alijiunga na jeshi la Nchi hiyo na kuwa mmoja wa maafisa wa jeshi,alifanya kazi kwa karibu na mkuu wa intelijensia wa jeshi la nchi hiyo na kupanda vyeo ambapo baada ya Omar Torrijo ambaye ndiye aliyekua mkuu wa intelijensia wa jeshi kufanya jaribio la mapinduzi na kushinda alipewa nafasi hiyo mwaka 1968.Baada ya kifo cha torrijo mwaka 1981,Norriega alijiimarisha kiutawala mpaka akawa kiongozi wa panama ingawa sio rasmi mwaka 1983 (de facto ruler of panama). kuanzia mwaka 1950 mpaka karibu na kipindi ambacho Marekani walikuja kumvamia, Norriega alikua akifanya kazi kwa karibu sana na C.I.A. Norriega alikua moja ya vyanzo muhimu vya kuamnika vya C.I.A. kwenye masuala ya intelijensia, pia ilikua ndio sehemu muhimu ya kuanzishia, kupanga pamoja na kupitishia silaha na fedha linapokuja suala la operasheni yoyote inayohusu masuala ya kijeshi marekani ya kati na kusini.

Norriega pia alijihusisha na biashara ya madawa ya kulevyahas cocane kwa kiwango cha hali ya juu kitu ambacho wamarekani walikifahamu fika kwa miaka mingi, ila waliliruhusu suala hilo liendelee kwa sababu za umuhimu wa Norriega kwenye masuala ya kijeshi na kiusalama katika ukanda huo wa marekani ya kati na kusini.

Utawala wa Norriega katika Nchi hiyo uligubikwa na ukandamizwaji wa vyombo vya habari, uimarishwaji wa jeshi, pamoja na uteswaji na ukandamizwaji wa mahasimu wa kisiasa. Noriega aliweza kusimamia uchaguzi wowote na kupata matokeo anayotaka yeye, alijitengenezea utajiri mkubwa kupitia biashara yake ya madawa ya kulevya. Taratibu mahusiano yake na Nchi ya marekani yalianza kupungua kwa sababu ya vitendo hivyo pamoja na kuanza kuuza taarifa za kiintelijensia kwa mahasimu wa marekani. Mwaka 1988 Norriega alibainishwa kwamba ni mmoja wa watu wanaosafirisha madawa ya kulevya katika miji ya Miami Florida. Marekani waliiivamia Panama 1989 na kumuondoa madarakani na kumpeleka marekani kama mfungwa wa kivita.

alisomewa makosa nane yanayohusiana na kuuza madawa ya kulevya kupanga na kusafirisha madawa ya kulevya na utakatishaji wa fedha haramu. Mwaka 1992 alihukumia kifungo cha miaka 40 jela mbapo kilipunguzwa na kuwa miaka 30 jela. 

Kifungo cha Norriega nchini marekani kilisitishwa mwaka 2007 baada ya Nchi ya Panama pamoja na Ufaransa kuomba kumuhukumu bila yeye mwenyewe kuwapo mahakamani kwa mauaji mwaka 1995 na utakatishaji wa fedha mwaka 1999. ufaransa ilikabidhiwa mtuhumiwa huyu mwaka 2010 mwezi wa nne baada ya ombi lao kukubaliwa na alifikishwa Paris 27|4|2010 na baada ya kesi yake kusikilizwa upya alihukumiwa kifungo cha miaka saba, mwezi wa saba 2010. Makubaliano ya kumhamisha gereza kutoka Ufaransa na kumpeleka Panama kutumikia kifungo cha miaka 20 yalifikiwa ikiwa ni vifungo vyote vilivyomkabili nchini marekani pamoja na ufaransa hivyo alipelekwa panama 23|09|2011. Norriega alifariki katika hospitali ya Santo Thomas katika jiji la Panama 29|05|2017 miezi miwili baada ya uperation ya ubongo.

MAISHA YA MWANZO NA FAMILIA

Noriega alizaliwa katika jiji la panama,katika familia ya kimasikini ya mestizo au mchanganyiko wa rangi ambayo inajumuisha wazawa wa marekani,waafrica na waspaniola.Mama yake anazungumziwa kuwa mpishi na dobi na baba yake alikua muhasibu na hakuishi muda mrefu na mama yake alifariki kwa maradhi ya kifua kikuu wakati Noriega akiwa mdogo.Noriega alilelewa na bibi yake katika apatimenti ya chumba kimoja katika makazi ya watu wengi holela (slum) za mji wa Terraplen.Waandishi wa habari na wa vitabu wanasema kwamba sio mtoto halali wa Ricaurte Noriega bali ni mtoto wa house boy wao ambaye uinasadikiwa alitembea na mama mwenye nyumba ,houseboy huyo alijulikana kwa jina la Moreno.

Norriega alipata elimu yake ya mwanzo Escuela República de México, na baadae katika shule ya sekondari inayoheshimika sana jijini Panama kwa kuzalisha wanamapinduzi wengi na viongozi wa kisiasa ya Instituto Nacional . Akiwa katika shule hizi alikua naelezewa kama kijana ambaye yuko makini muda wote. Pia anaelezewa kama kijana aliyependa sana kusoma na alikua anavishwa vizuri na mlezi wake.

wakati akiwa Instituto Nacional, alikutana na kaka yake luis ambaye ni nduguyake na alikua mwanaharakati katika shule hiyo ,norriega kabla ya hapo hakuwahi kukutana na ndugu wa kuzaliwa kwa upande wowote sio mama wala baba. Huyu Luis ndiye hasa alimleta Norriega kwenye siasa na kumpeleka kwenye chama cha kijamaa upande wa vijana. Kuna wakati alikua akiishi pamoja na kaka yake. Wakati akiwa katika chama hicho upande wa vijana alishiriki katika maandamano na pia kuandika baadhi ya makala ya kukosoa uwepo wa Mrekani katika Panama.Katika wakati huu ndio inasadikiwa kwamba ndipo wamerekani walimchukua katika kitengo chao cha intelijensia na alikua akitumiaka katika kuwapa taarifa wamarekani za kikundi cha wanaharakati wenzake akiwemo kaka yake. aliendelea kufanya kazi na wamerekani katika sehemu mbalimbali mpakamwaka 1980 na inasadikiwa aliwahi kulipwa kiasi cha usd 10.70 mwaka 1955 ambapo ilikua ni moja ya malipo ya awali ambayo aliendelea kulipwa kwa mda mrefu kwa kutoa taarifa hizo.

Baada ya kumaliza katika shule ya Instituto Nacional alipata scholarship kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Chorrillos Military School kilichopo Nchini Peru mjini Lima kwa kusaidiana na Luis ambaye tayari alikua anafanya kazi katika ubalozi wa panama nchini Peru.Alikua na ndoto zilizoota mbawa za kuwa daktari ila alishindwa kupata nafasi katika chuo kikuu cha Panama. Akiwa nchini peru alitengeneza urafiki na Roberto Díaz Herrera, ambaye baadae alikuja kuwa rafiki wa karibu na muhimu sana.

Norriega baadae alioana na Felicidad Sieiro de Noriega, ambaye walikutana mwaka 1960 na walifanikiwa kupata mabinti watatu ambao ni Lorena, Sandra and Thays Noriega. Siero alikua ni mwalimu wa shule na Norriega alikua mwanajeshi. familia ya mkewe Norriega haikufurahishwa na ndoa hiyo, pamoja na hayo Norriega anaonekana hakuwa na utulivu katika ndoa yao na mara kadhaa mkewe alisikika akitaka ndoa hiyo ivunjwe ingawaje baadae alibadili mawazo na kuendelee na mumewe. wahusika hawa wanne wa familia hii ya Norriega wanaripotiwa kwamba walikuwepo wazima wa afya wakati wa kifo cha Norriega.


Imeandikwa kwa msaada wa mtandao wa Wikipedia

ITAENDELEA........

IJUE APPLICATION YA "TEAM VIEWER" ITAKAYOKUSAIDIA KUBADILISHANA MAFAILI, VIDEO, NYIMBO, KUONGEA, KUFANYA MIKUTANO UKIWA MBALI NA MHUSIKA NA HATA KUTATUA TATIZO LAKO LA KOMPUTA AU SIMU UKIWA MBALI NA MTAALAMU WAKO.

Na Josephat Keraryo Nyambeya .
nyambeya@yahoo.com
how to use teamviewer
Hii ni program ya komputa ambayo inafanya kazi za kushea mafaili, kuhamisha mafaili (file ssharing), mikutano ya mbali (online meetings), msaada wa kikomputa hata ukiwa mbali kati ya komputa na komputa. Program hii ya team viewer inakupa uwezo wa kuifikia komputa nyingine bila kuwa karibu na komputa hiyo, mfano unaweza kuingia kwenye omputa ya mtu aliyepo Marekani, Mwanza, Australia, Kigoma, Nairobi au sehemu yoyote ya dunia bila wewe kuwepo sehemu hiyo. Mfano unaweza kuhamishiana mafaili na mtu aliyepo Kigoma huku wew ukiwa Mtwara kwa Dangote bila usumbufu wowote, unaweza kufuta kitu chochote kwenye komputa ya mtu uliyeingia kwenye komputa yake kwa kutumia hiyo hiyo Team Viewer.

Watu wengi haswa makampuni yenye maboss wasio na utambuzi mzuri wa komputa au matawi mengi mikoani na sehemu mbalimbali za dunia huitumia program hii ya Team Viewer kuwasiliana na wataalamu wao wa IT pale wanapokumbana na matatizo.
TEAM VIEWER INAFANYAJE KAZI?

Ili program hii ya Team Viewer ifanye kazi sharti uipakue kwenye mtandao na kuiingiza kwenye komputa au simu yako. Na pia unaetaka kuwasiliana nae aiingize kwenye simu au komputa yake , na mtakapoanza kutaka kufanya kazi (mikutano ya mtandaoni, kushea mafaili, kuelezana shida na mambo yote inayoyafanya team viewer) wote mnatakiwa muwe hewani na muifungue kwa program hii , kisha mmoja atabonyeza sehemu inayomtaka aunganishe na program hii moja kwa moja itawasiliana na itakuletea namba ambazo utamtajia mwenzako aliyepo mbali na wewe kisha ataziingiza kwenye huko huko kwenye Program yake zikiingiliana tu basi kila mmoja wenu ataanza kuiona komputa au simu ya mwenzake na kila kilichomona mtaanza kushea mafaili. Kama mnataka kuongea basi mtapitia njia hizo hapo juu na mawasiliano yataenda sawa bila shida.

WAPI INAFANYA KAZI?
Program ya team viewer inafanya kazi kwenye mifumo ya ANDROID , WINDOWS, LINUX, MAC OS, BLACK BERRY, IoS na kadhalika nakadhalika.

Team viewer ilitengenezwwa na wataalamu wa mawasiiano mwaka 2005 huko nchini Ujerumani kabla haijanunuliwa na kampuni moja la Kingereza mwaka 2014.
Kwa ufupi hayo maelezo yanatosha kukupa mwanga juu ya programu hii, usisikitike kama wewe ni mpenzi wa Muvi, nyimbo, picha, video za ngono, mahubiri, kaswida, au chochote na unamjua mwenye nacho ila huwezi kumfikia au kuzipata kwa sababu ya umbali mwambie aanze kutumia team viewer, ili akutizimie hitaji la roho yako.

Post hii imeletwa kwa hisani ya www.technbraino.blogspot.com ...Usisite kuitembelea bog hiyo ili ujipatie ufahamu wa mambo ya kidunia, kiteknolojia, kitaaluma ili ukuze ubongo wako.



NIKOLA TESLA:: MWANASAYANSI NGULI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI

Alizaliwa Ulaya Mashariki kwenye nchi ambayo leo ni Croatia/Serbia. Kipindi ambacho kulikuwa na option mbili tu Kujiunga na Jeshi au dini. Baba yake alikuwa ni Mchungaji wa kanisa na mama yake alikuwa mama wa nyumbani. Alilazimishwa kujiunga na kanisa lakini alikataa hakuwa tayari. Mama yake kakuwahi kwenda shule lakini alikuwa na talent ya kushona na uwezo mkubwa wa kukariri mashahiri vitu vilivyomfanya mtoto Tesla kuvutiwa sana.Vitu hivi vilimfanya kuwa na uwezo wa kufanya hesabu ngumu za CALCULUS (watu wa Hisabati mnanielewa) kwa kichwa kitu kilichowafanya waalimu wahisi anadanganya au kunasehemu anaangalizia.

MAISHA YA AWALI

Akiwa mtoto mdogo aliposoma kuhusu maporomoko ya Niagara Marekani kichwani mwake aliona Gurudumu likizunguka katikati ya maji. Kwa immagination na meditation akajakuwa founder wa umeme wa maji miaka mingi baadae alipofika hilo eneo. 

Kuna kipindi akiwa chuo alikuwa akisoma kuanzia saa tisa usiku hadi saa tano usiku mfululizo. Hadi siku moja akiwa nyumbani akakuta barua ya siri ya Proffesor akimuandikia baba yake wamrudishe nyumbani maana akiendelea atafariki.


KISA CHA KWENDA MAREKANI

Akiwa na upenzi wa sayansi alipata kazi katika viwanda. Baadae alienda Ujerumani alipopata kazi kisha akaajiriwa na kampuni ya kimarekani ya umeme DC General Electric ya Thomas Edison founder wa DC current. (Umeme wa DC hutolewa sana na Betri).

Waliokuwa na tawi Ufaransa. Kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha akapata transfer kwenda makao makuu ya kampuni hiyo Marekani afanye kazi ya kudesign na pia atakuwa karibu zaidi na Edison.
Akaingia New York akiwa bado kijana sana.



KUTOKA KUWA MTAALAMU HADI KUCHIMBA MITARO KAMA KIBARUA
Akifanya kazi bila kuchoka, akifanya design, siku moja bosi wake Edison alimuambia akidesign system ambayo itasaidia kuboresha ufanisi wa mashine zake atapewa dora 50 ambayo ilikuwa pesa nyingi kwa wakati huo. Alipofanikiwa jamaa akamgeuka akamwambia alikuwa anamtania. Jamaa akaamua kuacha kazi hata baada ya kulazimishwa saana. Alichokutana nacho ni maisha magumu kupita kiasi. Ilifika kipindi akawa anachimba mitaro, ili angalau apate pesa ya chakula. Hadi siku moja alipojiuliza kwa nini anafanya kazi za ajabu huku kichwani anaazina ya kutosha.


MVUMBUZI WA AJABU 

Alikutana na jamaa ambao aliingia nao makubaliano ya wao watamsupport ktk vitu anavyokuwa akivumbua. Uvumbuzi wa DC motor alioufanya na baadae kuwa mshauri kwa kampuni pinzani ya Edison. Alijipatia pesa nyingi maana kwa uvumbuzi wake ulilingizia kampuni hilo mamilion ya pesa. Kitu ambacho kilihatarisha uhai wa kampuni yake aliyoacha kazi ya Mr Edison. Alikuwa halali zaidi ya masaa manne.fedha hizo aliziingiza katika utafiti wake huku akiishi hotelini maisha yake yote hadi mauti inamkuta.



VITA VYA UMEME
Wivu wa uvumbuzi wa umeme mbadala wa edison ulimfanya jamaa kutumia fitna kuwatisha watu kua umeme huo ni hatari saana kwa uhai.

Edison alikusanya watu newyork akafanya maonyesho ya hatari. Kuua tembo, nyani kwa umeme wa AC. Watu walijaa hofu. Tesla yeye aliwaita watu waje washuhudie jinsi alivyoweza kuzungusha yai bila kupasuka juu ya sahani kwa kutumia AC motor. Siku Edison aliponyamazishwa rasmi ni pale alipowanyima akina Tesla haki ya kutumia taa zake Za DC siku maalumu ambapo watu walitoka dunia nzima kuja kushuhudia uvumbuzi mwingine wa Tesla. Tesla aliishangaza New York nzima, usiku ulipofika akiwasha taa zake mwenyewe kwa umeme wake ambao ulifunika jiji zima. DC bulbs zikaonekana kama koroboi. Mji ukawa kama mchana.



MAAJABU YA KISAYANSI
Aliweza kutengeneza radi hata ndani ya chumba alichokuwa anafanyia utaafiti.

Alijenga mnara kwa mara ya kwanza alitaka umeme uwe wireless. Dunia nzima iwe na umeme bila hata waya.
Alipotengeneza wireless controlled boat waalikwa wa siku ya maonyesho waliona ni uchawi. Wakasema kuna nyani mdogo kamtrain ndio anaendesha baadae wakafungua hawakukuta kitu.
Akasema awauzie jeshi la marekani hiyo technology wakamdharau lkn leo mabomu,drones na vitu karibu vyote wireless huwezi kumsahau Tesla. Mnara wa kwanza wa mawasiliano ulijengwa na huyu jamaa japo kwa lengo la kutransmit power alifanikiwa kupokea signal kwa mara ya kwanza zikitokea ulaya. Huku yeye na wenzake walidhani zimetoka mbinguni au sayari tofauti.



ANATUFUNDISHA NINI UNAPOTEGEMEA KITU KIKUBWA GHAFLA MKASA WAAJABU UNAKUPATA (usikate tamaa)
Akiwa katikati ya Uvumbuzi na utafiti wa X-RAY(ambayo baadae wakati akiwa na hili tatizo jamaa mwingine akavumbua) katika maabara yake, Hakuamini macho yake kesho yake asubuhi alipokuta maabara yake imeungua na kila kitu kimekuwa ni majivu tu. tesla alipoteza Mamia ya ,

1. Documents za mipango yake,
2. Design zake zote alizokuwa ameziandaa,
3. Notes , invention models
4. Picha zake alizokuwa amejitunzia pamoja na vitu ambayo alikuwa ameviandaa tayari kwa maonyesho.

Alipoteza kiila kitu, vitu vyote vilikuwa na thamani zaidi ya $50,000 miaka hiyo, alipoulizwa na gazeti ya New York times kuhusu janga lililompata, kwa huzuni na uchungu alisema, "I am in too much grief to talk, What can I say?", lakini alijikongoja akaanza upya kwa kuwa supported na sponsors waliomuamini na akafanya mambo makubwa zaidi ikiwepo wireless radio wave driven boat.


KUFA MASIKINI HUKU AKIACHA MAMBO YALIYOWAACHA WENGI MABILIONEA
Pamoja na mambo makubwa aliyofanya nikola tesla alikufa akiwa hana kitu. Alifia hotelini alipokuwa akiishi. Kazi kubwa aliyoifanya iliishia kuwafanya kuwa mabilionnaire. Mfano mwanasayansi wa italia Marconi ilipata tenda na patent kutoa huduma ya fax marekani baada ya kumshinda kesi Tesla. Lakini kiukweli karibu kila alichotumia ni ideas za Tesla na mfadhili wake Morgan akaamua kumuacha na kumsupport Marconi. Vitu karibu vyote alivyovumbua viliishia mikononi mwa wanasayansi makanjanja na kujitajirisha. Tatizo lake hakujielekeza kwenye haki miliki na pia yawezekana wamarekani hawakutaka kumpa umaarufu japo alichukua uraia. Kama angekuwa umiliki wa uvumbuzi wake leo. Angekuwa tajiri namba moja duniani maana krb kila kitu cha sasa anamkono wake.

AMEKUFA LAKINI KAACHA ALAMA ZA KUDUMU DUNIANI IKIWA NI MATUNDA YA MATUMIZI SAHIHI YA UBONGO WAKE.
Miaka ya sitini Tesla ilipitishwa kuwa SI unit ya Magnetic flux density (wale wa Physics Advance wananielewa) kumuenzi. Amekuwa kivutio kwa wanasayansi vijana enzi hizo akiwapo Albert Einstein ambaye anamuona kama role model. Baada ya kufa inasemekana makachelo wa marekani waliofika hotelini hapo waliondoka na mavumbuzi mengi yake ya kijeshi ndio maana wako vizuri kivita baada ya kudevelop.
Mfano wanasayansi leo wanafanya utafiti wa kusambaza umeme dunia nzima kupitia anga linaloitwa Ionosphere. Marekani wanafanya research ya kutumia reflecting satelite kupeleka umeme Japan. Zote hizo ni kazi za tesla zilizomfanya akaitwa Mwanasayansi KICHAA.
Baadhi ya vitu vilichukuliwa na ndugu zake zikapelekwa serbia na yawezekana wanasayansi wa urusi walitumia pia kudevelop vitu na silaa. Mitaa, vyuo, mabarabara, vikundi vya wasomi, taasisi za kisayansi vimeitwa kwa jina lake kumuenzi Great thinker huyu katika mambo ya science na technolojia.

Imeandikwa na MSEZA MKULU wa Jamii Intelligence

HILI BOMU NDIO MFALME WA MABOMU YOTE KUWAHI KULIPULIWA ULIMWENGUNI, NDILO BOMU HATARI ZAIDI DUNIANI.

Tumekuwa tukisikia mabomu mabomu tokea tunaanza kujitambua hadi sasa , ila ni kwa mara chache tumepata kujiuliza uzito na uhatari wa mabomu hayo. Katika makala hii ninakuletea kiufupi bomu hatari zaidi kuwahi kutengenezwa na mikono ya mwana wa Adamu. 

Mwanzoni mwa miaka ya 50 na 60 dunia ilishuhudia mpasuko mkubwa baina ya Mashariki na Magharibi, kipindi hiki  ndio kilikuwa cha kupona vidonda baada ya kutoka kujeruhiwa na Vita kuu ya pili ya dunia, vita ambayo mtata Adolf Hitler aliihenyesha dunia, vita ambayo kwangu mbabe huyu wa Kijerumani ninampa "credit" kwa kuionyesha dunia umahiri wake na commitment yake aliyokuwa ameiweka ili kuifanya Ujerumani kuwa super power duniani. Baada ya Ujerumani kuangushwa katika vita hii mataifa ya Marekani na Urusi kwa upande mwingine yaliwagombania wataalamu na Wanasayansi wa Ujerumani na kuwamishia katika nchi zao ili wakahamishie utaalamu wao katika nchi zao. Oparesheni hii ilipewa jina maarufu la "Paperclip". Katika oparesheni hii Marekani iliwakusanya wataalamu, wahandisi na wanasayansi zaidi ya 1600 wa Kijerumani na Urusi pia iliwachukua wengi. 

Image result for tsar bomba
Bomu la TSAR BOMBA likiwa katika moja ya kambi yake jijini Moscow-Urusi mwaka jana kama lilivyonaswa na shirika la habari la Sputnik.


Katika Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa (United Nations General Assemby) wa mwaka 1960, Rais wa Urusi kipindi hicho bwana Nikita Khrushchev aliikemea Marekani kwa maneno makali na kuahidi kuwaonyesha kuwa Urusi ni nani. Baada ya ahadi hiyo Bomu zito la TSAR BOMBA lilianza kuzaliwa katika mawazo ya wanafizikia wa Kirusi waliokuwa kwa wingi wamechukuliwa kutoka Ujerumani baada ya kuanguka kwa utawala wa Hitler pamoja na wanasayansi wenyeji wa Urusi walianza kazi maabara ya kuzalisha kitu cha aina yake duniani. 


Bomu hili liliandaliwa kuwa likilipuka litoe mlipuko wa uzito wa Megatoni (Tani Millioni) 100 lakini baada ya kukamilika liliweza kulipuka katika na kutoa mlipuko wa uzito kiasi cha Tani millioni 50, watalaamu wanasema kama lingeweza kuachiwa kulipuka kwa intensity ya tani milioni 100 basi lingeweza kuipasua dunia katika vipande viwili mithili ya yai na hivyo kuiathiri hata Urusi yenyewe. 


TSAR BOMBA, ni bomu la Hydrogeni, mlipuko wake ni mara 1570 zaidi ya muunganiko wa milipuko ya mabomu ya Atomiki  yaliyopigwa na Marekani katika jimbo la Hiroshima na Nagasaki. Can you imagine how heavy and deadliest is this bomb?


Bomu la TSAR BOMBA wakati linafanyiwa majaribio mwaka 1961 lilibebwa na ndege maalumu ya kijeshi iliyotengenezwa kwa ajili ya kulibeba, rubani aliyeiendesha ndege hiyo maalumu ili kufanikisha zoezi hilo alipandishwa cheo baada ya zoezi hilo na kupewa tuzo ya shujaa wa Urusi.
Bomu hili lina urefu wa mita 8 na kipenyo cha mita 2.1, wakati wa majaribio lilipangwa kudondoshwa kutoka urefu wa Km 10 angani , wingu zito la moshi wake ulipaa angani km 64, mara 40 zaidi ya urefu wa mlima Everest ambao ni mrefu zaidi ulimwenguni.


Cheche zake ziliruka umbali wa Km 1000 kutoka lilipodondoshewa, yaani ni sawa bomu lilipuliwe Dar es Salaam halafu cheche zake ziruke hadi kufika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza. Hatari sana. Hiyo ilikuwa mwezi Oktoba mwaka 1961.


Mtikisiko wa bomu hili hatari ulisikika bara zima la Ulaya, na kuathiri baadhi ya nchi zikiwemo Norway, Finland na nyingine. Vijiji vya jirani na eneo la mlipuko viliathiriwa vibaya kwa nyumba zao kubomoka . Mlipuko wake wazidi kishindo cha tetemeko la ardhi.


TSAR bomba ndilo bomu zito na hatari zaidi kuwahi kutengenezwa na mikono ya mwanadamu.


Uzito wa bomu hili ni tani 27.  Mawimbi ya mlipuko huu yaliizunguka dunia mara tatu, dakika arobaini ya kulipuka kwa bomu hili mawimbi ya redio yalizimika kabisa kilomita elfu kadhaa kutoka eneo la mlipuko, hii ni kutokana na moshi wa bomu hili kuathiri anga za juu (Atmosphere).  Hii kwa lugha rahisi ni sawa na kusema Televisioni, Redio, na vifaa vyote vinavyotumia mawimbi ya redio vilizimika kwa muda hadi hapo anga ilipokuja kutengemaa baada ya moshi mzito wa bomu hili kusambaa. 

HII NDIO Tu-160 NDEGE (BOMBER) HATARI YA KIVITA INAYOUMIZA VICHWA VYA MAADUI..

Na Josephat Keraryo Nyambeya.
tu160_2.jpg
Kama nilivyoahidi juzi baada ya kutoa uchambuzi kiduchu juu ya bomber (B-2) ya Marekani nilisema nitakuja na uchambuzi kiduchu juu ya Tu-160 kutoka Urusi ili kuleta balansi juu ya ushindani uliopo kati ya hawa mabwana .Leo ningependa kuendelea na ule uandishi wangu kiduchu juu ya masuala mbalimbali kama ilivyo kawaida yangu siku zote. Leo ninapenda kujikita kwenye ndege vita aina ya Bombers lakini leo nitakuwa ninaijadili ndege vita hatari sana kutoka Urusi ambayo inaumiza watu vichwa haswa upande wa Magharibi (USA+NATO) kwa jinsi ilivyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu, japo wafuatiliaji na wachambuzi wa mambo ya Kijeshi na Teknolojia za ndege wanadai kuwa ile Bomber (B-2 niliyoijadili juzi ndio hatari zaidi duniani).

Tu-160 (Tupolev Tu-160) ikijulikana kama Blackjack kwa wanachama wa NATO ilianza kutengezwa kipindi cha vita baridi. Ndege hii ilitengenezwa na Tupolev and Kazan Aircraft Production Associatio Bomber hii hatari ya kivita ilitengenezwa kwa lengo moja kuu la kuweza kuzivamia na kuzishambulia sehemu muhimu za Marekani. Ikiwa inafanana sawa sawa na B-1B ya Marekani, hii ndio ndege vita (Bomber) nzito kuliko zote duniani ikiwa na uzito wa tani 275. Ndege hii inaweza kubeba silaha za kivita (Mabomu, Vichwa vya Nyuklia, Makombora ya kushambulia) yenye uzito wa Tani 40. Naomba ifahamike kuwa hakuna ndege vita aina ya Bomber kwa upande wa Marekani yenye kuweza kubeba silaha nzito namna hiyo kwa sasa labda kama ipo kiwandani ikitengenezwa (kwa Marekani B-1Bndio inabeba silaha za uzito wa tani 34) na kama nilivyotangulia kusema ni kuwa Tu-160 ilitengenezwa kuja kushindana na B-1B ya Marekani. Inaaminika kuwa jumla ya ndege vita hizi 39 zilitengenezwa lakini kutokana na gharama kubwa za uendeshaji na matunzo Jeshi la Wanahewa la Urusi linasadikika kuwa na jumla ya ndege hizi 16 tu kwa sasa. Na zipo aina nane za ndege hii.

Tu-160 ilipaa kwa mara ya kwanza mwaka 1981 na baada ya kuona haijakidhi matakwa kama walivyotarajia wahandisi wa ndege hii waliingiza tena kwenye sevisi mwaka 1987. Tu-160 inaweza kufanya kazi katika hali yoyote ya hewa, mchana, usiku na ina operate katika latitude zote za Kijografia. Ina mfumo wa kuijaza mafuta ikiwa angani na pia ina injini nne za Turbofan. Inakimbia kwa mwendokasi wa kilomita 2220 kwa saa.

Tu-160 ina mfumo wa kubeba makombora ya masafa marefu ya kushambulia aina ya Kh-55 na Kh-15. Pamoja na mambo mazuri iliyona nayo ndege hii hatari ya kivita bado ina mfumo hafifu wa rada. Hivyo kuwapa uwezekano maadui wa kuiona kwenye rada zao. Tu-160 kumi na tisa zilibaki nchi Ukraine baada ya kuvunjika kwa muungano wa Kisoviet (USSR) mwaka 1991, Urusi ilijitahidi kuzirudisha kwa makubaliano na Urusi hatimae ndege hizi 8 kati ya 19 zilirudishwa nchini Urusi mwaka 1999, na zingine zilizobaki zilifanywa Skrepa kwa makubaliano yaliyoongozwa na Marekani (Udhaifu huu). Kuanzia mwaka 2014 ndege hizi zinafanyiwa matengenezo na marekebisho ikiwemo kurekebisha mfumo wake wa radar , inategemewa kufikia 2020 ndege zote zitakuwa zimekamilika .Pia pamoja na marekebebisho hayo Urusi pia imeamua kutengeneza version mpya ya ndege hizi itakayojulikana kama Tu-160M2 ambayo itakuwa imara na ya kisasa zaidi yah ii iliyopo, project hii inaendelea kwa sasa na inatarajiwa kukamilika baada ya miaka michache tokea sasa. Marekani iliutumia udhaifu wa kuvunjika kwa Muungano wa Kisoviet kumrubuni mshirika wake Ukraine na kuzinyaka ndege tatu za Tu-160 na kuzigeuza kuwa Tu-16SK kwa ajili ya space vehicle launching.

Sifa zingine ilizonazo ndege hii ni kuwa inaweza kupaa angani kwa masaa 15 mfululizo bila kujazwa mafuta kama itakuwa inakimbia kwa kwa kasi ya kilomita 850 kwa saa, pia ina uwezo wa kujazwa mafuta tani 130 kwa mara moja. Inapaa umbali wa futi 30,003 sawa na mita 9145. Udhaifu wake mkubwa ni kuwa inaonekana kwenye RADA na kupaa umbali mfupi tofauti na B-2 ya Marekani ambayo haionekani kwenye rada na inapaa zaidi ya futi 50,000 juu. Mwaka 2010 ndege mbili za Tu-160 zilivunja rekodi ya kufanya Patrol ya masaa 23 mfululizo bila kutua ardhini.

Ifahamike kuwa kwa sasa Marekani wanaiboresha ndege yao (Bomber0 hatari ya B-2 na wanataka kuja na B-21 kama mbadala wa B-2 huku Urusi nao wakilenga kuja na Tu-160M2 kama mbadala wa Tu-160. Wenzetu hawalali, wanaumiza vichwa kutengeneza vitu vya kuvunja rekodi, sisi Tanzania na Afrika tunavunja rekodi ya kumezeshana Madesa tusiyoyatumia mara baada ya kuhitimu Elimu zetu, hivyo kujikuta tunabakia kuwa watumwa wa watu haswa wanasiasa badala ya kuwa sisi ndio dira yao, wanasiasa wanageuka kuwa Dira ya wataalamu kiduchu tulionao.
Older Posts
Powered by Blogger.
© Copyright TEKNOLOJIA KWANZA Published.. Yuvinusm
Back To Top