Imeandikwa na Josephat Keraryo Nyambeya kwa msaada wa mitandao wa kijeshi ya China na Marekani.
Kombora la DongFeng-41 (DF-41) ni kombora linalotengenezwa na kutumiwa na jeshi la China. Ni kombora la masafa marefu (mabara)., kwa kimombo waweza liita Inter Continental Ballistic Missile (ICBM).

Kombora la DongFeng-41 (DF-41) ni kombora linalotengenezwa na kutumiwa na jeshi la China. Ni kombora la masafa marefu (mabara)., kwa kimombo waweza liita Inter Continental Ballistic Missile (ICBM).

Lina uwezo wa kusafiri umbali wa kati ya Km 12,000 hadi
15,000. Umbali huu unaoweza fikiwa na DF-41 unalifanya kuwa kombora linaloenda
masafa marefu kuliko yote duniani na kulizidi lile la Marekani Minutemen
LGM-30, ambalo lina uwezo wa kufika Km 13,000. Km 13,000 ni sawa na umbali wa
Dar Es Salaam hadi New York ni Km 12,400 hivyo nadhani unaweza ona uwezo wa
makombora haya. Yaani kwa maana nyingine
makombora haya ya wababe hawa yanaweza fyatuliwa kutoka ncha ya kaskazini mwa
dunia yakafika ncha ya kusini mwa dunia bila shaka yoyote maana umbali kati ya
hizo ncha mbili ni Km 12,430. Makombora ya ICBM yana uwezo wa kugonga pembe
yoyote ya dunia bila shaka yoyote. Unaweza kulifyatua ukiwa chumbani kwako
likaenda kutua Sydney kule Australia bila wasi wasi. (anyway tuendelee).
Kombora la DF-41 ndilo kombora linaloaminika kuwa na kasi
kubwa kuliko makombora yote duniani, likiaminika kusafiri kwa kasi ya Km 30,626
kwa saa sawa na Maili 19,030 kwa saa au sawa na Km 8.5073 kwa sekunde. Hii
ikiwa na maana ya kwamba kombora hili linaweza kutoka Mbezi Africana jijini Dar Es salaam hadi ikulu ya Dar kwa
sekunde moja. Historia ya kuundwa kwa kombora hili ilikuwa mahsusi ili
kupambana na nguvu ya kijeshi na nyuklia ya Marekani.


Kombora la DF-41 lilijaribiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012.
SIFA ADIMU ZA DF-41
1.
Lina uzito wa tani 80
2.
Lina urefu wa mita 21 na upana wa mita 2.25
3.
Toa maoni yako juu ya habari hii. Pia usisahau kubonyeza matangazo yaliyopo juu na chini hata pembeni ya habari hii maana ndio wadhamini wanaonipa nguvu ya kuendelea kuandika, bila wao sitaweza kuandika.

Post a Comment