HILI BOMU NDIO MFALME WA MABOMU YOTE KUWAHI KULIPULIWA ULIMWENGUNI, NDILO BOMU HATARI ZAIDI DUNIANI.

Tumekuwa tukisikia mabomu mabomu tokea tunaanza kujitambua hadi sasa , ila ni kwa mara chache tumepata kujiuliza uzito na uhatari wa mabomu hayo. Katika makala hii ninakuletea kiufupi bomu hatari zaidi kuwahi kutengenezwa na mikono ya mwana wa Adamu. 

Mwanzoni mwa miaka ya 50 na 60 dunia ilishuhudia mpasuko mkubwa baina ya Mashariki na Magharibi, kipindi hiki  ndio kilikuwa cha kupona vidonda baada ya kutoka kujeruhiwa na Vita kuu ya pili ya dunia, vita ambayo mtata Adolf Hitler aliihenyesha dunia, vita ambayo kwangu mbabe huyu wa Kijerumani ninampa "credit" kwa kuionyesha dunia umahiri wake na commitment yake aliyokuwa ameiweka ili kuifanya Ujerumani kuwa super power duniani. Baada ya Ujerumani kuangushwa katika vita hii mataifa ya Marekani na Urusi kwa upande mwingine yaliwagombania wataalamu na Wanasayansi wa Ujerumani na kuwamishia katika nchi zao ili wakahamishie utaalamu wao katika nchi zao. Oparesheni hii ilipewa jina maarufu la "Paperclip". Katika oparesheni hii Marekani iliwakusanya wataalamu, wahandisi na wanasayansi zaidi ya 1600 wa Kijerumani na Urusi pia iliwachukua wengi. 

Image result for tsar bomba
Bomu la TSAR BOMBA likiwa katika moja ya kambi yake jijini Moscow-Urusi mwaka jana kama lilivyonaswa na shirika la habari la Sputnik.


Katika Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa (United Nations General Assemby) wa mwaka 1960, Rais wa Urusi kipindi hicho bwana Nikita Khrushchev aliikemea Marekani kwa maneno makali na kuahidi kuwaonyesha kuwa Urusi ni nani. Baada ya ahadi hiyo Bomu zito la TSAR BOMBA lilianza kuzaliwa katika mawazo ya wanafizikia wa Kirusi waliokuwa kwa wingi wamechukuliwa kutoka Ujerumani baada ya kuanguka kwa utawala wa Hitler pamoja na wanasayansi wenyeji wa Urusi walianza kazi maabara ya kuzalisha kitu cha aina yake duniani. 


Bomu hili liliandaliwa kuwa likilipuka litoe mlipuko wa uzito wa Megatoni (Tani Millioni) 100 lakini baada ya kukamilika liliweza kulipuka katika na kutoa mlipuko wa uzito kiasi cha Tani millioni 50, watalaamu wanasema kama lingeweza kuachiwa kulipuka kwa intensity ya tani milioni 100 basi lingeweza kuipasua dunia katika vipande viwili mithili ya yai na hivyo kuiathiri hata Urusi yenyewe. 


TSAR BOMBA, ni bomu la Hydrogeni, mlipuko wake ni mara 1570 zaidi ya muunganiko wa milipuko ya mabomu ya Atomiki  yaliyopigwa na Marekani katika jimbo la Hiroshima na Nagasaki. Can you imagine how heavy and deadliest is this bomb?


Bomu la TSAR BOMBA wakati linafanyiwa majaribio mwaka 1961 lilibebwa na ndege maalumu ya kijeshi iliyotengenezwa kwa ajili ya kulibeba, rubani aliyeiendesha ndege hiyo maalumu ili kufanikisha zoezi hilo alipandishwa cheo baada ya zoezi hilo na kupewa tuzo ya shujaa wa Urusi.
Bomu hili lina urefu wa mita 8 na kipenyo cha mita 2.1, wakati wa majaribio lilipangwa kudondoshwa kutoka urefu wa Km 10 angani , wingu zito la moshi wake ulipaa angani km 64, mara 40 zaidi ya urefu wa mlima Everest ambao ni mrefu zaidi ulimwenguni.


Cheche zake ziliruka umbali wa Km 1000 kutoka lilipodondoshewa, yaani ni sawa bomu lilipuliwe Dar es Salaam halafu cheche zake ziruke hadi kufika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza. Hatari sana. Hiyo ilikuwa mwezi Oktoba mwaka 1961.


Mtikisiko wa bomu hili hatari ulisikika bara zima la Ulaya, na kuathiri baadhi ya nchi zikiwemo Norway, Finland na nyingine. Vijiji vya jirani na eneo la mlipuko viliathiriwa vibaya kwa nyumba zao kubomoka . Mlipuko wake wazidi kishindo cha tetemeko la ardhi.


TSAR bomba ndilo bomu zito na hatari zaidi kuwahi kutengenezwa na mikono ya mwanadamu.


Uzito wa bomu hili ni tani 27.  Mawimbi ya mlipuko huu yaliizunguka dunia mara tatu, dakika arobaini ya kulipuka kwa bomu hili mawimbi ya redio yalizimika kabisa kilomita elfu kadhaa kutoka eneo la mlipuko, hii ni kutokana na moshi wa bomu hili kuathiri anga za juu (Atmosphere).  Hii kwa lugha rahisi ni sawa na kusema Televisioni, Redio, na vifaa vyote vinavyotumia mawimbi ya redio vilizimika kwa muda hadi hapo anga ilipokuja kutengemaa baada ya moshi mzito wa bomu hili kusambaa. 

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
Powered by Blogger.
© Copyright TEKNOLOJIA KWANZA Published.. Yuvinusm
Back To Top