
Na Josephat Keraryo Nyambeya.
Kuna aina nyingi za meli vita duniani, kama Keria, Kruza, Distoyazi na nyinginezo. NIMITZ ni aina meli Keria. Katika aina hizi za meli za Keria NIMITZ ndio meli hatari zaidi duniani.
NIMITZ ndio meli kubwa zaidi duniani yenye uwezo wa kubeba ndege vita 90 . Ina uwezo wa kubeba zaidi ya tani 100,000 za mizigo ya kivita. NIMITZ ni aina ya Melivita aina ya Keria yenye uwezo mkubwa sana wa kujilinda na mashambulizi kutoka upande wa adui, NIMITZ pia inabeba vichwa vya Nyuklia ikiwa na uwezo wa kufyatua makombora ya nyuklia ya masafa marefu.
Melivita hii ya NIMITZ inamilikiwa na jeshi la wanamaji la Marekani (US Navy) , kwa taarifa yako Melivita ya NIMITZ inaendeshwa kwa nguvu ya Nyuklia hivyo ina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 20 mfululizo bila kujazwa mafuta. (20 years).
Ujenzi wa melivita moja hii ya NIMITZ uligharimu Dollar Bil 4.5 za Kimarekani sawa na Trillioni 9.2 za Kitanzania, Kwa sasa Jeshi la Wanamaji la Marekani linazimiliki Melivita hizi 10 tu. Meli vita hii moja aina ya NIMITZ ina uwezo wa kuendesha vita dhidi ya nchi bila kuhitaji msaada wa wanajeshi wengi kutoka Marekani, kwa maana ya kwamba Mashambulizi yatakuwa yatakuwa yanappangwa na kutokea humo humo, ikiwemo ndege kutua na kuruka kutokea huku.
Melivita hii inatumika kama kiwanja cha ndege cha kijeshi kwa ajili ya ndege hizo kutua na kuruka kwenda kumshambulia adui. Ina urefu wa mita 333 . NIMITZ inakimbia kwa spidi ya Kilomita 56 kwa saa. NIMITZ ina mfumo wa kisasa zaidi ya kujilinda dhidi ya Makombora ya maadui,pia siyo rahisi kushambuliwa kutoka ndege za maadui au meli vita nyingine.

NIMITZ zipo katika bahari mbalimbali duniani zikiangalia usalama wa Marekani. Zipo katika bahari ya Meditrania, Pasifiki, Atlantiki na bahari nyingine. Hivyo kuifanya Marekani kuweza kuwa na uwezo wa kumshambulia adui kutoka Meli ya NIMITZ bila kupeleka majeshi yake kwenye ardhi ya adui.
NIMITZ zinatarajiwa kubadlishwa na FORD carrier kama mbadala wa NIMITZ ambazo zinategemewa kuingia kazini kuanzia mwaka 2025, Utengenezaji wa Ford umekwisha anza na unatarajiwa kumalika mwaka 2023/2024. FORD carriers zitakuwa zaidi ya NIMITZ, Teknolojia inazidi kupanuka.

3 comments
Bravo asee America ipo juu, pata picha Nchi kama Tz tunawachokoza America nadhan watatuletea meli hyo moja tu na tutapigwa balaa, haha lol
Replyhongera kwa kufungua blog
Replyhongera brother kwa kufungua blog
ReplyPost a Comment